Safari za ujasiriamali hazifanani, na kila mfanya biashara ana sababu na motisha tofauti za kufanya kile anachofanya.
Hata hivyo, karibu kila mtu ambaye ameamua kujiajiri atathibitisha ni kwamba ujasiriamali ni safari ya mafunzo ya muda mrefu na kwamba kuwekeza katika elimu kunawawezesha wajasiriamali kufanikiwa
Kweli, hauitaji digrii kutoka kwenye chuo kikuu maarufu kuchukua hatua zako za kwanza katika uuzaji wa moja kwa moja. Lakini, hakuna njia moja kwa moja ya mafanikio ya ujasiriamali. Na kutokana na mabadiliko mengi inamaanisha wamiliki wa biashara wanapaswa kujizatiti na ujuzi sahihi , kukua na kustawi.
Kwa kuzingatia hilo, hapa kuna faida nne za kujifunza kwa kuendelea na kwa nini QNET – kupitia jukwaa letu la kujifunza qLearn – daima imekuwa ikiweka kipaumbele na kuhimiza elimu ya ujasiriamali.
Maarifa ni nguvu kwako na kwa biashara yako
Iwe wewe ni mgeni au mfanyabiashara mkongwe, kutafuta uhuru wa kifedha kunaweza kuwa changamoto. habari njema ni kwamba karibu kila kipindi kigumu kinaweza kuboreshwa kwa maarifa.
Kadiri ujuzi unavyopatikana, ndivyo mambo yanavyokuwa rahisi zaidi, kuanzia kutengeneza mipango ya uuzaji hadi kusimamia fedha na wanachama wa timu.
Maarifa pia huwasaidia wajasiriamali kufanya maamuzi ya akili, kuwahamasisha wale walio karibu nao na kuelewa mambo tofauti, magumu ya biashara, hata viwanda vinavyoonekana kutohusiana na uuzaji wa moja kwa moja.
Kwa mfano, mtu anaweza kufikiria kuwa uhalifu wa mtandao hauna uhusiano wowote na sekta yetu. Bado QNET, ikiwa ni kampuni ya uuzaji wa moja kwa moja ya biashara ya kielektroniki, imekuwa ikizingatia kwa muda mrefu teknolojia na uvumbuzi. Kwa hivyo, kujiandikisha kwenye programu ya qLearn’s Cyber Security na IT, kwa mfano, kunaweza kuruhusu wajasiriamali kufahamu thamani ya ulinzi wa data na usimamizi wa taarifa.
Elimu hukusaidia kukabiliana na mabadiliko
Sio tu kwamba mwelekeo wa biashara hubadilika mara kwa mara, lakini pia hali za kimataifa.
Wepesi wa ujasiriamali, hata hivyo, ni zaidi ya kuwa tayari kubadilika. Pia inasaidia kuweza kumudu mazungumzo na matarajio magumu nay a ghafla. Wamiliki wa biashara wanahitaji kujitayarisha na ujuzi husika, ambao ndio mafunzo kama vile qLearn’s Agile Management husaidia kufanya.
Ukuaji wako unaweza kuathiri vyema biashara yako
Mjasiriamali ni moyo na roho ya biashara yake. Na ingawa hicho ni kitu chanya, pia inaweza kumaanisha kwamba wakati mwingie uhisi wewe na biashara yako kukwama katika hali mbaya.
Kinyume chake, unapozingatia ukuaji wa kibinafsi, hiyo huleta kufanikiwa. Zaidi ya hayo, ikiwa unajifunza na kufanya kazi kwa bidii kwa wakati mmoja, unaweza pia kutumia maarifa mapya uliyopata kwa shughuli zako za biashara.
Hii ndiyo sababu moduli nyingi za mafunzo ya kielektroniki za qLearn zimeundwa ili kuruhusu wajasiriamali wanafunzi kutekeleza kile wamejifunza mara moja.
Kujifunza kunatoa jukwaa la upanuzi
Mbali na matumizi ya mara moja ya ujuzi uliopatikana hivi karibuni, maarifa mapya yanaweza pia kusaidia kuweka msingi wa upanuzi wa biashara yako.
Kama Mwakilishi Huru wa QNET (IR), unaweza kuamua jinsi ya kuendesha biashara yako na wakati wa kupanua shughuli. Hata hivyo, mipango madhubuti kama vile Certified Network Marketer+, ambayo inaruhusu wajasiriamali kujifunza kutoka kwa wataalam waliobobea wa kimataifa, inaweza kukusaidia kukuongoza kuhusu kile kinachofaa na kisichopaswa kufanywa.
Kimsingi, wamiliki wa biashara wanapaswa kuzingatia mambo mengi kabla ya kupanua shughuli, ikiwa ni pamoja na kuandaa timu zao, kuhakikisha kila mtu yuko sawa na kuweka mifumo. Kwa hivyo, viongozi lazima waboreshe ujuzi wao na wajifunze mambo bora zaidi ya dhana kama vile kuhifadhi na kurudia kabla.
Kwa kifupi, kuwa mjasiriamali ni zaidi ya kuamua kumiliki biashara. Badala yake, ni juu ya mageuzi ya mara kwa mara na thabiti. Na kujipatia maarifa sahihi kunaweza kukutayarisha wewe na biashara yako kwa siku zijazo.