Afisa Mkuu wa Habari wa QNET (CIO) Ivan Woo alijiunga na Mkutano wa Microsoft Cybersecurity Summit 2021 huko Hong Kong kama sehemu ya jopo la wataalamu na wenye sauti kuu kuhusu usalama wa mtandao. Jopo lililenga kupunguza hatari za mtandaoni na kuimarisha usalama mtandaoni kwa mwaka mpya ujao. Kutokana na Covid-19, hali mseto za kufanya kazi zimewaweka watu kwenye hatari za usalama mtandaoni. CIO wa QNET alikuwa mmoja wa watu wachache ambao utaalamu wao ulitafutwa ili kujadili matatizo na kupata ufumbuzi wa pamoja.
Mkutano wa Microsoft Cybersecurity ni Nini?
Ukiwa umeandaliwa Hong Kong, Mkutano wa Microsoft Cybersecurity 2021 ni jukwaa linalolenga kuelewa mbinu na mienendo bora ili kuweka watu na mashirika salama kutokana na hatari za usalama mtandaoni. Wanajopo hao ni pamoja na watu wazito wa tasnia kama vile Mshauri Mkuu wa Usalama wa Mtandao wa Microsoft na Afisa wao wa Kitaifa wa Teknolojia, na CIO wetu, Ivan Woo. Walijadili mikakati dhidi ya vitisho vya ndani na mbinu za kulinda mali yako ya kidijitali.
Majadiliano ya Jopo Na Afisa Mkuu wa Habari wa QNET Ivan Woo
Kama mtu anayesimamia utendaji wa Global IT na Uzoefu wa Dijitali katika QNET, Ivan alichaguliwa kama mwakilishi kamili wa jopo, ili kuangazia ushirikiano wa Microsoft-QNET.
CIO wa QNET iliongoza mijadala kuhusu vipaumbele muhimu vya kua usalama mtandaoni mwaka 2022, na jinsi ya kukaa salama katika ulimwengu wa mseto wakati wengi wetu wamelazimika kufanya kazi nyumbani. Ameongoza mipango kadhaa muhimu ya mabadiliko ya kidijitali katika QNET ambayo ilijumuisha uhamiaji wa kutumia teknolojia ya “Cloud”, utekelezaji wa mkakati wa kwanza wa simu za mkononi, na mipango madhubuti ya usalama wa data, akilenga katika kuhakikisha wasambazaji wetu sio tu wanapata uzoefu bora wa biashara ya mtandaoni, lakini pia usalama zaidi.
Kuhusiana na mtazamo wa QNET kuhusu usalama, Ivan ana haya ya kusema “pamoja na karibu familia zetu zote za QNET, washirika, na wateja kulazimishwa kukumbatia mtandao kwa mahitaji yao, watu wa IT lazima wajitokeze na kuchukua majukumu ya uelimishaji. Wanapaswa kueleza hatari na kuwaelimisha watumiaji kuhusu umuhimu wa usalama mtandaoni na jinsi ya kuchukua hatua ili kuwa salama. QNET inaelewa hili na tutaendelea kuchukua hatua kuelekea kuhakikisha kwamba tunashughulikia misingi yote katika masuala ya ulinzi na usalama mtandaoni