Kuna njia nyingi za kuelekea kwenye mafanikio ya biashara, na magwiji wa kuuza moja kwa moja wanatambua kuwa miongoni ya yote, kujenga uhusiano na wateja ni muhimu kwa mafanikio.
Lakini iakuaje ikiwa mtu si wakujichanganya na wengine na ana matatizo ya kuanzisha mazungumzo? Au vipi ikiwa mteja anayemtarajia kaondoka? Je, unawezaje kutafuta kujenga urafiki na, hivyo basi, kupata mauzo?
Hatua nzuri ya kwanza ni kuwa mwaminifu katika mtazamo wako na kuzingatia maswali au mada ambazo zitakusaidia kuunda uhusiano thabiti na kukuza uaminifu.
Hapa kuna vianzilishi vitano vya mazungumzo ili kukuongoza:
Matukio
Bila kujali historia, uzoefu au ujuzi, sote tunaathiriwa na mambo mengi. Lakini badala ya kuzungumzia hali ya hewa, ambayo inaweza kuonekana kuwa ya kawaida, kwa nini usijaribu kuzungumzia tukio la hivi karibunu kwenye vyombo vya habari?
Ndiyo, masuala ya rangi, dini na siasa, ambayo ni nyeti na yanaweza kusababisha mijadala mikali, yanapaswa kuachwa mezani. Lakini hakuna sababu kwa nini vipengele kutoka kwenye kurasa za Habari za michezo, biashara au mtindo wa maisha, haziwezi kutumika kama kianzilishi cha maongezo
Kidokezo, ingawa, umuhimu ni kufanya utafiti kabla na kuzingatia mada ambazo zinaweza kuwavutia wateja wako. Unaweza kuangalia kurasa zao za mitandao ya kijamii, haswa wasifu wao wa LinkedIn, kwa vidokezo.
Mapendeleo
Kama ilivyo kwa matukio ya kiujumla, ni rahisi kuunganishwa na vitu sawa. Lakini kwa nini usizungumze kuhusu matarajio yako au matamanio ya mteja badala ya yako mwenyewe?
Watu hupenda kuzungumza juu ya kile wanachopenda zaidi, iwe ni maslahi ya muda mrefu au hobi mpya. Kwa hivyo, zingatia kuuliza kuhusu jinsi wateja wako wanavyotumia muda wao wa bure na Maisha baada ya mida ya kazi, kwa mfano.
Ndio, haya yanaweza kuonekana kama maswali ya kukimbia. Lakini kama vile magwiji wa mauzo wamegundua, kuzama katika mambo yanayompendeza mtu kunaweza kutumika kama ufunguo wa kuungana nao kwa maana zaidi.
Familia, Marafiki na Wanyama
Kama kanuni ya jumla, mazungumzo ya mauzo yanapaswa kuachana na mambo binafsi. Lakini, watu wengi wanaovutiwa na uuzaji wa moja kwa moja hufanya hivyo ili kuhakikisha maisha bora kwa wapendwa wao.
Kwa hivyo, maadamu una heshima, hakuna ubaya kuzungumzia mambo ya kibinafsi na kupendezwa na familia ya mteja, au hata Wanyama wao.
Bila shaka, familia inaweza kuwa swala nyeti kwa baadhi ya watu. Kwa hivyo, inashauriwa kuanza polepole, kwa maswali mepesi kama, “Una ndugu wangapi?” au “Je, una watoto/Mpenzi?” Majibu ya wateja wako yataonyesha kama wangependa kuzungumza zaidi. Ila Kuwa tayari kuendelea na mada nyingine.
Hadithi na matukio ya kutia moyo
Kila mtu anapenda hadithi nzuri, na katika biashara, hadithi inayovutia zaidi, ni bora zaidi. Kwa hivyo, kwa nini usisimulie hadithi nyingi za mafanikio za QNET na uzungumze na matarajio wako na wateja kuhusu hizi?
Hadithi zinaweza kunasa mawazo ya msikilizaji, kufanya ujumbe kuwa wazi zaidi na kutoa taswira ya kile kinachowezekana. Kwa hivyo, kutumia shuhuda chanya za wajasiriamali na wateja wa QNET bila shaka kutawapa ufahamu bora zaidi wa QNET pamoja na bidhaa na huduma zetu.
Hata hivyo, usijisikie kulazimishwa kusimulia hadithi yako katika biashara. Hakika, RYTHM Foundation ina hadithi nyingi sana za matumaini na za kutia moyo ambazo watu wanapaswa kujua.
Mada za Kufikirisha
Ingawa mada zenye utata, kwa ujumla, hasipaswi kuzungumziwa, unapofahamiana na wateja wako na matarajio, zingatia mada zinazoweza kusababisha mijadala ya wazi zaidi na ya uhuru
Ni kweli, maswali kama vile “Unahisije kuhusu ujasiriamali?” na “Maoni yako ya awali ya kuuza moja kwa moja yalikuwa yapi, na yamebadilikaje?” huenda isikusaidie kuzalisha mauzo na mikataba Hata hivyo, majibu unayopata yanaweza kutoa maarifa muhimu kwa ajili ya kujenga uhusiano wenye nguvu zaidi kati ya muuzaji na mteja. Bora zaidi, unaweza kuondoa sintofahamu flani.
Mwisho wa siku, ingawa, yote ni juu ya kile kinachokijia kwa urahisi. Kwa hivyo, usikatae njia yako, sikiliza kwa makini, zingatia mtu aliye mbele yako na, muhimu zaidi, jitahidi kuwa mwaminifu.