Waongozaji wa biashara za mtandaoni Asia,QNET imetangaza mipango ya kupanua shughuli zake katika soko la Kenya. “Soko la Kenya, Uganda na Tanzania tayari lina idadi kubwa ya wateja na kutokana na ongezeko la uhitaji wa vituo vya usambazaji mtandaoni, uwezekano unabaki kuwa mkubwa kwa QNET kukuza uwepo wake wa Afrika Mashariki, “alisema Meneja wa Maendeleo ya Biashara wa QNET Muqtadir Suwani
Akizungumza kwenye kituo cha watoto yatima cha Ramisi Markar watoto ambapo wawakilishi huru wa kampuni hiyo walitoa chakula na vifaa vya thamani ya mwezi mmoja kukidhi mahitaji ya yatima wasiopungua 60 katika mji wa pwani wa Mombasa, Kenya.