Watanzania wametakiwa kuchangamkia biashara za mitandaoni kutokana na ukuaji wa teknolojia ya habari na mawasiliano inayowezesha upatikanaji wa bidhaa kwa urahisi duniani kote.
Msechu, mkufunzi katika chuo cha mauzo na masoko katika Chuo cha Access jijini Dar es Salaam, anaitaja kampuni ya QNET akidai nayo imeonekana kufanikiwa katika masoko ya mtandao ikifanya mauzo ya moja kwa moja. “Ni kweli, biashara ya mtandao nchini Tanzania bado iko katika hatua ya maendeleo, hata hivyo bila shaka inauwezo wa kukua haraka,” alisema.