QBUZZ
  • BIDHAA
    • Saa na Vito
    • Afya
    • Elimu
    • HomePure
    • Huduma Binafsi
    • Likizo
    • Ustawi
  • MAFANIKIO
    • Hadithi za Mafanikio
    • Mapigo ya tasnia
    • Uuzaji wa kitaalamu
    • Vidokezo vya Mafanikio
  • HABARI
    • Matukio
    • Taarifa kwa Umma
    • Tuzo
  • MICHEZO
    • Muktasari
    • Uanamichezo
    • QNET City
  • RYTHM
    • Maendeleo
    • Urithi wa kijani
    • Usawa wa kijinsia
  • MAJIBU YA QNET
Reading: Mafunzo ya usimamizi kutoka kwa Umoja wa Mataifa
Notification
  • Africa (SW)
    • Africa (FR)
    • Africa (EN)
    • OTHER REGIONS
      • Global (EN)
      • RCIS (RU)
      • MENA (AR/FR)
      • Indonesia (ID)
      • India (EN)
      • Turkey (TR)
QBUZZ

EN | FR | SW

Font ResizerAa
  • BIDHAA
  • MAFANIKIO
  • HABARI
  • MICHEZO
  • RYTHM
  • MAJIBU YA QNET
Search
  • BIDHAA
    • Saa na Vito
    • Afya
    • Elimu
    • HomePure
    • Huduma Binafsi
    • Likizo
    • Ustawi
  • MAFANIKIO
    • Hadithi za Mafanikio
    • Mapigo ya tasnia
    • Uuzaji wa kitaalamu
    • Vidokezo vya Mafanikio
  • HABARI
    • Matukio
    • Taarifa kwa Umma
    • Tuzo
  • RYTHM
    • Maendeleo
    • Urithi wa kijani
    • Usawa wa kijinsia
  • MICHEZO
    • Muktasari
    • QNET City
    • Uanamichezo
  • VIUNGO VINAVYOHUSIANA
    • Majibu ya QNET
    • Lexicon
    • Seti ya Zana
    • Jiandikishe
    • Chapisho la sauti
    • QNET 25
    • Webilearn
    • Hifadhi
  • MIKOA MINGINE
    • Global (EN)
    • RCIS (RU)
    • MENA (AR/FR)
    • Indonesia (ID)
    • Turkey (TR)
    • India (EN)
  • English
  • French
  • Swahili
QBUZZ > Habari > Matukio > Mafunzo ya usimamizi kutoka kwa Umoja wa Mataifa
HabariMatukio

Mafunzo ya usimamizi kutoka kwa Umoja wa Mataifa

Last updated: 2021/11/17 at 7:03 AM
QNET Official
Share
6 Min Read
Jumuiya ya Ulimwengu
Jumuiya ya Ulimwengu
SHARE

Tuliadhimisha Siku ya Umoja wa Mataifa. Siku hii Huadhimishwa kilavtarehe 24 Oktoba kila mwaka. Ni siku ya inayoadhimisha siku Umoja wa Mataifa ulianza rasmi.

Contents
Kuwa na maono yaliyo waziKubadilika na kua na maelewano ni jambo la msingiUfanisi kwenye mawasilianoHakuna kitu kama mafanikio ya mara mojaVipande vyote ni muhimu

La muhimu pia, niku sherehekea jinsi shirika la miungano ya serikali imekuwa na jukumu muhimu katika kuhifadhi amani ya kimataifa kwa karibu miongo minane.

Ilianzishwa mwaka 1945 baada ya Vita Kuu ya Pili ya Dunia ikiwa na nchi 51 kama wanachama, ujumbe wa Umoja wa Mataifa namba (1) moja ulikuwa kuleta ulimwengu pamoja na kupiga vita ukatili wa vita na ukiukwaji wa haki za binadamu.

Katika miaka 76 tangu kuanzishwa kwake, imebadilika na kukua, kupanuka wigo wake.

Kwa hiyo, ni jinsi gani shirika ambalo kwa sasa linajumuisha nchi 193  zenye tamaduni, itikadi, na lugha tofauti, kufaulu kufanya kila mtu kufanya kazi pamoja katika ulimwengu unaobadilika haraka?

Na sisi kama wauzaji wa moja kwa moja tunawezaje haswa katika ulimwengu unaozidi kutokuwa na mipaka, tujifunzaje kutoka kwa shirika hili kubwa jinsi ya kupata ushindi katika ulimwengu wa biashara? Yafuatayo ni mafunzo matano kutoka kwa Umoja wa Mataifa ambayo yamehakikishiwa kukuweka katika nafasi nzuri:

Kuwa na maono yaliyo wazi

Miaka sabini na sita ni muda mrefu. Na UN imelazimika kurekebisha, kuelekeza, na hata kubadilisha malengo yake mengi kama shirika.

Hata hivyo, daima huzingatia madhumuni yake manne ya msingi – kudumisha amani na usalama wa kimataifa; kuendeleza mahusiano ya kirafiki kati ya mataifa; kufikia ushirikiano wa kimataifa; na kufanya kazi ili kuoanisha matendo ya mataifa.

Kufanikiwa katika biashara, kama ilivyo katika maisha, mara nyingi ni juu ya kudumisha umakini wa dhati juu ya malengo yako maalum.

Je, ni vipi  shirika ambalo limelazimika kushughulika na migogoro kama mauaji ya halaiki ya Rwanda na, hivi majuzi zaidi, COVID-19, kuendelea kujikwamua kutokana na changamoto na hata makosa?

Kubadilika na kua na maelewano ni jambo la msingi

Kukiwa na takribani  ya nchi zenye wanachama 200, migogoro ina hakika kutokea. Hata hivyo, Umoja wa Mataifa daima umetafuta ufumbuzi wa pamoja ambao unafanya kazi kwa kila mtu na kwa manufaa zaidi ya ubinadamu.

Kupata suluhisho la pamoja haijawahi kuwa rahisi. Na kwa kawaida, hata mwanzoni, kulikuwa na ugomvi kuhusu eneo la makao makuu yake. Kwa hivyo, jiji la New York lilipochaguliwa kuwa mji mwenyeji wa Umoja wa Mataifa, uamuzi ulifanywa kwamba mashirika fulani ya Umoja wa Mataifa yangebaki Ulaya. Maelewano.

Unyumbufu huu na kujua wakati wa kuafikiana ni muhimu kwa uhai wa shirika, na vile vile kungesaidia biashara yako vyema.

Ufanisi kwenye mawasiliano

Kuhamasisha kampeni nyingi za usaidizi na za kulinda amani juu ya kuandaa mikutano ya kimataifa kunahitaji maelfu ya wafanyikazi kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi.

Ni jambo dogo kusema kwamba Idara ya Mawasiliano ya Umoja wa Mataifa ina jukumu muhimu katika kuhakikisha kila mtu anajua ni wapi anastahili kuwa na kile anachopaswa kufanya.

Na ingawa wauzaji wa moja kwa moja wanaweza kuwa na mitandao midogo zaidi kuliko UN, mkakati mzuri wa mawasiliano na wanachama wa timu na wateja utatumika tu kuimarisha ukuaji wa mtaalamu wa masoko.

Hakuna kitu kama mafanikio ya mara moja

Hakika, Umoja wa Mataifa umejaribu mara nyingi tangu kuanzishwa kwake. Lakini, kumbuka, hakuna hata moja ya haya yaliyotokea mara moja.

Kwa kweli, ilichukua miaka kwa shirika hilo hata kuanzisha mashirika muhimu kama vile Shirika la Afya Ulimwenguni na Mpango wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa.

Watu wengi huingia kwenye uuzaji wa moja kwa moja, wakiamini vibaya kwamba mafanikio ni rahisi kupatikana. Lakini kama vile kujenga shirika la kimataifa, ukweli ni kwamba ushindi katika biashara unahitaji muda na juhudi.

Kunaweza kuwa na hatua zenye changamoto na kujikwaa njiani. Jambo kuu, hata hivyo, kwa mjasiriamali yeyote ni kukaa kwenye njia yake na kuwa na subira.

Vipande vyote ni muhimu

Mara nyingi wakati wa kuzingatia Umoja wa Mataifa, mtazamo usio na uwiano unawekwa kwa nchi kama China, Ufaransa, Urusi, Uingereza, na Marekani; mataifa matano yenye mamlaka ya kura ya Turufu katika baraza la usalama. Lakini wakati nchi hizi zina mamlaka makubwa juu ya masuala ya usalama, shirika linatoa fursa sawa kwa kila mtu.

Kwa mfano, Shirika la Chakula na Kilimo, lililojikita katika kutokomeza njaa, lilianzishwa katika Jiji la Quebec, na sio mojawapo ya Mataifa Matano makubwa, bali kufuatia msukumo mkubwa kutoka kwa serikali ya Canada.

Somo hapa ni kwamba kila mtu katika shirika lako ni muhimu, kuanzia kwa wale wenye viwango vya juu  na viongozi hadi wale wanaoanza tu kama wawakilishi huru.

Weka imani yako kwa watu, kama UN, hivi karibuni utaona biashara yako ikizawadiwa vikubwa.

You Might Also Like

Jinsi Bidhaa ya QNET zinavyoonyesha Kuwawezesha na Kuhamasisha Watu Binafsi na Jamii

QNET Yaonya Umma Kuchukua Taadhari Dhidi ya Ulaghai wa Usafirishaji Haramu wa Binadamu nchini Sierra Leone

Heri ya Miaka 26 ya Mafanikio, Familia ya QNET!

QNET Yatoa Ufafanuzi Wa Mfumo Wa Biashara: Biashara Halali Sio Mpango Wa Ponzi

QNET iliendesha maonesho ya Bidhaa huko Lagos, Ikionesha Kujitolea kwa Ubunifu na Uwezeshaji

TAGGED: Mafunzo ya usimamizi, Malengo endelevu ya umoja wa mataifa, qnetpro, Ujasirimali, Umoja wa Mataifa, Uuuzaji wa moja kwa moja
Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Telegram Copy Link
Previous Article Kindess ukarimu tija Sio tu wema: Biashara ya wema
Next Article mikakati ya uuzaji wa moja kwa moja Mikakati ya Mafanikio kwa Wauzaji wa Moja kwa Moja
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Gundua Bidhaa za QNET

Habari mpya kabisa

QVI Vacay App
Gundua Safari Yako Ifuatayo na QVI Vacay App!
Likizo December 5, 2024
Maonyesho ya QNET
Jinsi Bidhaa ya QNET zinavyoonyesha Kuwawezesha na Kuhamasisha Watu Binafsi na Jamii
Matukio November 12, 2024
QNET Yazindua Bernhard H. Mayer Wave Rider
QNET Yazindua Toleo La Kipekee La Bernhard H. Mayer Wave Rider: Kito Cha Usahihi Na Matukio
Saa na Vito November 6, 2024
EDG3 Plus
Kuwezesha Afya Ulimwenguni: QNET wahamasisha Ubora wa Lishe katika Siku ya Chakula Duniani 2024
Afya October 29, 2024

Endelea kushikamana

17k Followers Like
3.5k Followers Follow

Endelea Kusasishwa kila wakati

Jiandikishe kwa jarida letu ili kupata nakala zetu mpya mara moja!

Jiandikishe
Facebook Instagram Telegram Twitter Youtube
MIKOA MINGINE
  • Global (EN)
  • RCIS (RU)
  • India (EN)
  • Mena (AR)
  • Turkey (TR/AR)
  • Indonesia (ID)
KANUSHO
  • Sera ya faragha
  • Kanusho
  • Masharti ya matumizi
  • Sera ya mitandao ya kijamii
  • Kanuni za maadili

© 2024 QBUZZ | Sauti ya QNET. Haki zote zimehifadhiwa.

Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?
  • Swahili