Wakati huu tayari umeshapanga zawadi nzuri na kuiandaa siku yake kua ya kipekee na kumpa wakati mzuri Mama yako. Kinachokosekana ni kadi nzuri ya kumuonyesha jinsi unampenda. Iwe unasherehekea na mama yako mzazi au wanawake ambao ni kama mama kwako, Wakati huu ni muafaka kumshukuru kwa ujumbe mzuri wa kutoka moyoni. Ikiwa unajitahidi kuweka kwa maneno ni kwa kiasi gani mama yako anamaanisha kwako, tumeandaa orodha yenye jumbe nzuri za Siku ya Mama Duniani.
Jumbe maalumu
Mama yako hawezi kubadilishwa, ni mkamilifu kwa njia yake yaki pekee. Muda wote hua nyuma yako akikuongoza na kuhakikisha kila kitu kinaenda sawa bila kujali nyakati au muda.
Hizi ni jumbe za kipekee ambazo unaweza kutumia kumuambia mama yako jinsi unampenda kwa moyo wako wote.
- Kuwa mtoto wako ilikuwa bahati nzuri, lakini kuwa na wewe kama rafiki yangu wa karibu ilikuwa chaguo. Asante kwa kuwa pale kwa ajili yangu kila hatua ya njia. Ulinilea, uliniunga mkono na unanikubali vile nilivyo. Ninajivunia kuwa na wewe kama mama yangu.
- Ninataka kuchukua muda leo kukujulisha kwamba si shukuru tu kwa ajili yako, pia nakupenda kwa moyo wangu wote. Ikiwa nikabahatika kua hata nusu ya mtu kama wewe, nitakua mwenye furaha Zaidi duniani.
- Umekuwa na ushawishi mzuri sana maishani mwangu. Ubunifu, shauku, uelewa – kuna mengi ya kujivunia juu yako. Asante kwa kujitoa kwangu wakati wote. Daima utakua wa kuigwa.
Ujumbe wa Kufurahisha
Ikiwa hupendelei kutumia njia ya hisia, ongeza ucheshi kwenye ujumbe wako. Chagua moja ya salamu hizi kumfanya acheke.
- Mshauri, Dereva, Mwalimu, Mwamuzi, Rafiki, Mtaalam, Mpishi, Shujaa wa kiwango cha juu – Siku ya Leo natambua vyeo vyao vote.
- Katika Siku hii ya Mama duniani, ningependa kukushukuru kwa kazi nzuri iliyofanya. Hongera kwa kunifanya kuwa wa kipekee sana! -Nakupenda, mtoto wako unayempenda zaidi.
- Mpendwa mama, asante kwa kunivumilia haswa ikiwa ni mtoto mkorofi, mwenye kukasirisha, asiye na shukrani na mtundu kama ndugu yangu. Nawaombea msamaha, lakini angalau unae mimi. Nakupenda!
Nukuu za siku ya mama duniani
Ongeza uzito kwenye ujumbe wako kwa mama yako na nukuu hizi. Ikiwa mama yako anapenda za kuchekesha au hata zenye kuleta hisia nzuri moyoni, basi hizi nukuu zitamfaa.
- “Sio rahisi kuwa mama. Ingekua rahisi, baba wangeifanya ”- Dorothy, Wasichana wa Dhahabu
- “Mungu hakuweza kuwa kila mahali, na kwa hivyo aliumba mama.”- Rudyard Kipling
- “Mama yangu, ni mrembo, mtaratibu mwenye ukali wake, na mwenye mgongo wa chuma. Nikizeeka natamani kuwa kama yeye ”- Jodi Picoult
Awe ni mama anayefanya kazi, mama wa nyumbani, mama wa hiyari, mama wa mara ya kwanza, mama wa mbali, mama wa paka, mama wa mmea, bibi, mama wakufanania na mama, washauri au hata wanawake ambao ni Mama moyoni, hii ni fursa kwetu kumsherehekea mama na mwanamke yeyote kwenye nafasi hiyo. Tumia fursa hii kuwatumia mchanganyiko wa jumbe hizi ili Kuwaonyeshe jinsi unavyowapenda na kuwajali. Na kutoka kwetu QNET, Tunakutakia heri ya Siku Mama Duniani yenye Furaha. Tunakupenda na kukuthamini kuliko maneno yanaweza kusema!