Peleka mitandao yako ya kijamii kwenye viwango vipya ukitumia vidokezo hivi maalum vya Instagram Stories. Instagram Story kwa sasa ndiyo njia inayopendelewa na watu kuwasiliana kwenye mitandao ya kijamii, na kwa ujumla hupata maoni mengi kuliko picha za kawaida. Ikiwa uko kwenye Instagram lakini hutumii kipengele cha Story, unakosa baadhi ya fursa nzuri za kuleta watu wengi zaidi kwenye ukurasa wako. Hapa kuna vidokezo vya Insta Story.
Tumia Hashtag na weka majina ya maeneo (Location Tags)
Watu huchukulia kuwa Hashtag ni za maelezo tu, lakini kuzitumia kwenye Insta Story zako kutasaidia watumiaji wengine wanaopenda vitu sawa na wewe kukupata. Vivyo hivyo kwa kuweka majina ya mahali/maeneo- ikiwa watu wengi zaidi hutumia kutafiti usafiri, chakula kupitia njia hiyo. Wakati wowote unapo-post kwenye Insta Story yako zingatia kuweka Hashtag na eneo lako pia ikiwa inafaa.
Weka Instagram Story zako kwenye Vidokezo (Highlights)
Mojawapo ya vidokezo bora vya Insta Story ni kuhifadhi kwenye Highlights ikiwa kama sehemu ya vivutio. Lakini usihifadhi tu kawaida. Kwani Insta Story hupotea baada ya saa 24, ni muhimu kuzihifadhi ili watazamaji wako wazipate baada ya saa hizo 24 kuisha. Njia bora ya kufanya hivi ni kuchagua aina ya machapisho ambayo huchapisha mara kwa mara, na kuweka katika highlights maalum kwa ajili yao. Kwa mfano, hifadhi Hadithi zako zote za likizo chini ya kitengo cha “Safari” au hadithi zako za QNET chini ya “Kuuza Moja kwa Moja”.
Uliza Maswali na Uendeshe Kura
Tumia stika zote zinazopatikana kwenye programu yako. Sasa unaweza kushirikiana na Watazamaji wako kwa kutumia kipengele cha “Majaribio”, “Kura” au “Maswali” kwenye Instagram. Ni rahisi sana ku-post na kadiri unavyochapisha, ndivyo watu watakavyojihusisha zaidi. Shirikiana na watu wako katika kuunda orodha ya vitu vipendwa au fanya tu kura ya maoni kuhusu kile ambacho watu wanapendelea, na uone furaha inayofuata.
Waelekeze watu kwenye Tovuti Husika
Ikiwa unatumia kipengele cha Instagram Story kwa umakini zaidi, sasa wana chaguo la “Link” ambapo unaweza kutuma wafuasi wako kwenye tovuti sahihi. Ikiwa unashiriki habari muhimu au makala tu ambayo ungependa wafuasi wako waone, hakikisha kuwa unajumuisha “Link” kwa makala kamili ili waweze kusoma yote pia. Unaweza hata kuunganisha kwenye akaunti zako zingine za mitandao ya kijamii kama hii.
Shiriki Instagram Story Angalau Mara Moja Kwa Siku
Ufunguo wa kuwa na uwepo kwenye mistandao ya kijamii ambao hufanya tofauti ni kuwepo muda wote, angalau. Chapisha kwenye Instagram story kila siku, hata kama unachofanya ni kurudia mabacho ulishaweka. Shiriki Memes zako uzipendazo au ikiwa ungependa kuwa na mpangilio zaidi, unda kalenda ya mitandao ya kijamii na uchapishe mara kwa mara. Ni mojawapo ya vidokezo vya Instagram Story kutoka kwa wataalam ambayo inafanya kazi kwa kila mtu. Kadiri chapisho linavyoongezeka, ndivyo unavyoonekana kwenye kurasa za watu. Lakini, tahadhari, usichapishe kwa ajili ya kuchapisha. Chapisha kile unachopenda.
Shiriki Instagram story Kiotomatiki Kwenda Facebook
Hili ndilo jambo rahisi zaidi unaweza kufanya kwenye mitandao yako ya kijamii. Haijalishi ni wapi unashiriki na wafuasi wako wako wapi, unganisha akaunti zako mbili ili watazamaji wote waweze kufurahia maudhui yako. Shiriki Instagram Story hadi Facebook pia. Huhitaji kukumbuka kuifanya kila wakati, bofya tu shiriki kiotomatiki na uruhusu teknolojia ifanye kazi yote.
Kwa vidokezo hivi rahisi sana na rahisi kufuata vya Instagram Story,sasa unaweza kuongeza ushiriki kwenye wasifu wako ili wafuasi wako wahisi kuwa wameunganishwa nawe. Zaidi ya hayo, Instagram Story zinazovutia zinaweza pia kuleta watumiaji zaidi wanaotazama akaunti yako ili maelezo yako yaweze kufikia hadhira kubwa.
Tujulishe kwenye maoni ikiwa una maswali yoyote maalum kuhusu vidokezo vya Instagram story au Mitandao mingine ya kijamii, na tutaona ikiwa tunaweza kukupa ushauri zaidi. Usisahau kushiriki na marafiki na familia yako.