Kujumuika ni muhimu katika kujenga biashara. Ili kukuza kile unachotoa, lazima ukutane na watu na kuzungumza nao. Na ili kuunda timu nzuri, lazima ufanye vivyo hivyo mara kwa mara. Hii inaweza kuwa ya kutisha, haswa wakati unakabiliwa na wasiwasi wa kujumuika kijamii. Je, unatatizika kuanzisha mazungumzo, kupata marafiki wapya, au kuhisi wasiwasi kuhusu kuzungumza na mtu usiyemjua? Soma ili upate vidokezo vya kushinda wasiwasi wa kijamii na kupata ujuzi wa namna ya kukabili wasiwasi huo.
Wasiwasi wa Kijamii ni Nini?
Wasiwasi wa kijamii ni tofauti na haya. Ni woga wa muda mrefu na wakati mwingine mwingi wa hali ya kuogopa kujumuika na jamii, haswa na wageni au watu usiowajua. Kawaida huathiri kujiamini, mahusiano, na kazi, na kusababisha stresi katika hali ambazo hujazoea. Katika janga hili, watu zaidi na zaidi huripoti wasiwasi wanapopiga na kujibu simu na kukutana na watu wapya, haswa kwa kuwa tunaweza kufanya kila kitu kupitia maandishi na mtandaoni siku hizi.
Vidokezo vya Kushinda Wasiwasi wa Kijamii Katika Utafutaji
Hapa kuna vidokezo vya vitendo vya kujumuika ili uwe na nafasi nzuri zaidi ya kufanikiwa katika uuzaji wa moja kwa moja na QNET.
1. Tambua Wasiwasi Wako
Wasiwasi wa kijamii ni shida ya kawaida ambayo inakua rahisi kadri unavukua. Hatua ya kwanza katika kuponya na kudhibiti uwoga wako ya kijamii ni kuelewa kile mwili na akili yako inapitia unapohisi hivyo. Andika na ujitume ujumbe wa sauti kuhusu kile kinachoendelea akilini mwako, ni hisia gani za kimwili unazohisi, na unachohisi kinakusaidia katika hali kama hiyo.
2. Tenga muda Fulani wa kuwa na Marafiki
Miaka michache iliyopita ya kushughulika na janga imefanya hali za kijamii kuwa ngumu kidogo. Hii ni kweli hasa ikiwa unakabiliwa na wasiwasi wa kijamii au unategemea sana teknolojia ili kudumisha urafiki wako. Unapotangamana juu ya maandishi pekee, huwa unasahau mambo mafupi kama lugha ya kimwili na jinsi ya kufanya mazoezi ya kusikiliza kwa makini. Ili kuondokana na hali hiyo mbaya, nenda nje na marafiki zako mkutane ana kwa ana. Ifanye kuwa tabia. Maingiliano ya ana kwa ana ni muhimu.
3. Zoea hali ya kutokua sawa kila wakati
Kujiweka katika hali ambayo si ya kawaida itakusaidia kuwa na ujuzi wa kijamii. Kubali ukimya, jitolee ana kwa ana kukutana na watu usiowajua, na ujifunze kuzungumzia wasiwasi na mafadhaiko yako. Kumbuka tu kwamba kujianika kijamii ni ngumu hata kwa wale wanaojiamini zaidi – ujanja ni kufanya hivyo tu.
4. Yape changamoto Mawazo Yako Hasi
Ikiwa unatumia muda mwingi kuwa na wasiwasi juu ya njia zote ambazo mazungumzo au ushirikiano wa kijamii unaweza kwenda vibaya, jaribu kujisemesha mwenyewe kwenye kioo na kuelewa kwamba mawazo yako mabaya ni hofu tu inazungumza. Katika hali halisi watu wanatafuta uhusiano na mazungumzo. Inaweza kukutisha kujiweka nje, haswa kama muuzaji wa moja kwa moja. Yape hangamoto mawazo yako hasi kwa kufikiria ikitokea hali mbaya Zaidi,99% ya wakati, haiwi hivyo.
5. Kuwa Mkarimu Kwako mwenyewe
Mwisho wa siku wewe ni binadamu tu. Jitendee jinsi unavyowatendea wapendwa wako – kwa wema na uvumilivu. Fanya mambo katika maisha yako ambayo ni kwa ajili yako na wewe tu. Fanya mazoezi ya uthibitishaji wako kwenye kioo, tumia dakika chache kila siku katika ukimya, ukitafakari tu au fanya matembezi mafupi nje ili kuhisi kushikamana na kitu kikubwa kuliko wewe mwenyewe. Kumbuka kunywa maji ya kutosha, kula vizuri, na kupata usingizi wa kutosha. Wasiwasi unahusishwa sana na afya yako ya kiakili na ya mwili, kwa hivyo kujitunza ni muhimu. Fanya jambo moja kila siku linalokufurahisha.
Ikiwa una dalili kali za wasiwasi wa kijamii zinazoathiri ubora wa maisha yako, tafadhali tafuta usaidizi wa kitaalamu na matibabu.