Wakati madaktari wanazungumzia “mpangilio wa lishe bora”, wanasistiza kufuata na kushikilia mpango wa lishe bora. Siku hizi, hata hivyo, neno hilo huelekea kuhusishwa na lishe nyingi za mtandaoni. Lakini ingawa hizi zinaweza kukusaidia kupunguza uzito, lishe nyingi zisizodhibitiwa zinaweza kusababisha shida nyingi za kiafya.
Suluhisho bora ni kuachana na kufata mkumbo, pata ushauri kutoka kwa daktari, na kujiwekea sheria chache rahisi unazoweza kufuatisha.
Jambo la msingi ni kwamba huna haja ya kuruka mlo ili kudhibiti uzito wako. Unahitaji tu kujifunza kula, kunywa na kuishi bora.