QNET, kampuni ya mauzo moja kwa moja ya kimataifa inayojikita katika ustawi na mtindo wa maisha, hivi karibuni ilifahamishwa juu ya shughuli haramu zinazofanywa kwa jina la mkono wake wa CSR, RYTHM Foundation.
Mtu binafsi alianzisha ofisi huko Port Harcourt kwa jina la RYTHM Foundation na alikuwa akitoa matangazo mtandaoni ya kutoa kazi katika taasisi hiyo. Tukio hilo lilijulikana wakati mwombaji kazi aliambiwa kuwa alitakiwa kulipa ada ili kuhakikisha kupata kazi hiyo. Hofu ilimfanya mwomba ajira kuthibitisha uhalali wa tangazo kwa kuwasiliana na taasisi moja kwa moja.
QNET mara moja iliripoti tukio hilo kwa mamlaka husika, ambayo ilisababisha kukamatwa kwa mhusika, na suala hilo kwa sasa linafanyiwa uchunguzi. QNET ina wasiwasi mkubwa juu ya uigizaji wa RYTHM Foundation kwa shughuli haramu, ikiwa ni pamoja na kutoa kazi bandia na huduma zingine zs udanganyifu. RYTHM Foundation, QNET, au kampuni zetu tanzu, hazihusiani na shughuli hizi na zinakataa uhusiano wowote na wahusika. Kampuni inajitolea kushirikiana na mamlaka kufanya kazi kwa pamoja kumkamata mhalifu.
QNET inawaonya umma kuwa macho na kuthibitisha habari kabla ya kujihusisha na ahadi kama hizo.
QNET, na kampuni yoyote nyingine zinazohusiana, haizitoi kazi/ajira kwa malipo. Kampuni inawahimiza umma kuripoti matangazo kupitia laini ya WhatsApp ya kufuata sheria kwa masoko ya Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara kupitia +233256630005.
QNET inaendelea kuwa na dhamira ya kuwawezesha watu kupitia bidhaa zinazoboresha maisha na fursa za ujasiriamali mdogo mdogo. Kampuni imechukua hatua za elimu na ufahamu wa umma kama vile kuanzisha Kituo cha kutoa taarifa za udanganyifu katika Mauzo ya moja kwa moja (DSDC) na kuzindua “Kampeni ya Ufahamu wa Kijamii” na “Kampeni ya Sema Hapana” kulinda watu kutokana na udanganyifu.
Kituo cha Kutoa taarifa za udanganyifu katika Mauzo ya moja kwa moja – https://www.directsellingdisinformation.org/
Kampeni ya Sema Hapana – www.saynocampaign.org
QNET inathibitisha upya dhamira yake ya kudumisha imani na wateja, washirika, na jamii. Kampuni inaahidi kufanya biashara kwa uaminifu, uadilifu, na lengo la kuboresha maisha kupitia bidhaa zake na fursa za kibiashara.
Kwa habari zaidi, tembelea tovuti ya QNET kwa www.qnet.net au blogu yetu ya Afrika kwa https://www.qnetafrica.com/