Kusherehekea miaka 25 ya QNET ya kuwawezesha wajasiriamali – katika mazungumzo na Waanzilishi wa QNET Dato Sri Vijay Eswaran na Joseph Bismark.
Ulipoanza safari hii iliyozaa QNET, ni nini kilikuwa cha kwanza akilini mwako? Na uliwahi kufikiria ungefika hadi hivi?
DSVE: Hatukuanza kwa kuwaza kuanzisha kampuni kabisa. Wakati huo, hali zilikuwa kana kwamba tulikuwa na watu wapatao 1,500 katika timu yetu ambao walituheshimu, walikuwa wameweka imani yao kwetu na tulihitaji kufanya uamuzi kuhusu maisha yao ya baadaye. Kampuni tuliyoshirikiana nayo ilikuwa imefunga kazi usiku kucha na kutuacha tukiwa tumekauka. Kama viongozi, tulikuwa na jukumu kwa timu yetu. Hawa walikuwa watu wetu na walikuwa wametuamini kuwasaidia kubadilisha maisha yao. Tulijua hatungeweza kuwaangusha.
Jambo kuu akilini mwetu lilikuwa ni kuwajali watu wetu na kuwapa fursa ya kujenga maisha yajayo tuliyowaahidi. Tulikuwa kundi la watu wa asili tofauti tofauti. Nilikuwa peke yangu mwenye uzoefu wa usimamizi. Sidhani kama kuna hata mmoja wetu aliyeelewa kikamilifu kile ambacho kinahitajika ili kuanzisha kampuni lakini sote tulishiriki maadili sawa, na maono sawa, na hilo ni jambo la nguvu.
JTB: Tulipogundua kwamba kampuni tuliyoshirikiana nayo hayakua waminifu kwetu na imetuacha, mwanzoni nilikatishwa tamaa moyo sana. Sikujua tungefanya nini, lakini Vijay aliniambia niangalie hii kama fursa. Hatimaye, tulikuwa tumeanza safari hii ya mtandao wa masoko kwa sababu tulitaka kuwa huru kifedha na kuwa na udhibiti wa maisha yetu. Alidokeza kuwa bado tunaweza kuwa kwenye njia hii ya ujasiriamali, kwa mabadiliko machache tu. Tulipata fursa ya kuunda kitu kipya ambacho kingeshughulikia mapungufu ya kampuni zingine zote za uuzaji wa mtandaoni ambazo tulikuwa na uzoefu nazo hapo awali.
Hapo awali, niliogopa sana wazo la kuanzisha kampuni. Sikuwa na elimu rasmi, na sikuwa na uzoefu wa ushirika. Lakini, niliamuamini Vijay, na uwezo wetu pamoja wa kukabiliana na changamoto na kuzishinda. Kadiri nilivyofikiria juu yake, ndivyo nilivyopata shauku zaidi. Tulipata fursa ya kuanza upya na kwa masharti yetu wenyewe. Hiyo ilikuwa ni motisha kubwa. Bila shaka, nikitazama nyuma sasa, ninashangazwa na jinsi tulivyofika hapa.
Uuzaji wa mtandaoni ulikuwa tofauti kiasi gani mwaka wa 1998 na umeibuka vipi katika miaka 25 iliyopita?
JTB: Kanuni za kimsingi za uuzaji wa mtandaoni zimekuwa sawa kila wakati. Hii ni tasnia inayotegemea uhusiano na watu daima watakuwa rasilimali kuu ya biashara yoyote ya mtandao wa masoko. Kilichobadilika ni mbinu. Tangu siku za mwanzo wakati watu walibeba bidhaa kwenye gari zao na kutoka mkutano mmoja hadi mwingine, teknolojia ya leo imewawezesha watu kufanya biashara hii wakiwa majumbani kwao. Biashara ya mtandaoni, mCommerce, na mitandao ya kijamii imebadilisha kabisa jinsi unavyokutana na watu wapya na kuwasilisha bidhaa na biashara kwao. Biashara pia imekuwa isiyo na mipaka leo. Unaweza kukaa Cairo na kueleza manufaa ya bidhaa kwa mtu aliye Kolkata. Unaweza kuendesha mafunzo ya mtandaoni kupitia Skype na majukwaa mengine ya video bila kulazimika kusafiri kutoka sehemu moja hadi nyingine.
DSVE: Ulimwengu unagundua tena uuzaji wa mtandao kama aina ya ujasiriamali. Ingawa tasnia hii imekuwepo kwa zaidi ya karne, imekuwa ikipambana na mashaka. Tunaelekea wakati ujao ambapo teknolojia inafanya kazi nyingi za kitamaduni kuwa za kizamani. Tuna tatizo linaloongezeka la ukosefu wa ajira katika nchi nyingi, bila suluhu ya wazi kutoka kwa serikali yoyote. Zaidi ya vijana milioni 700 watahitimu kutoka vyuo vikuu na kujiunga na nguvu kazi ifikapo 2025 na hakutakuwa na ajira za kutosha kwao. Ujasiriamali ndio suluhisho pekee la kimantiki la kujaza pengo kati ya ongezeko la watu na kuongezeka kwa ukosefu wa ajira. Uuzaji wa mtandao ni moja wapo ya tasnia inayokua kwa kasi leo ambayo imeunda mamilioni ya wajasiriamali wadogo, na imenusurika majaribio ya wakati. Kilicho kizuri sana kuhusu tasnia hii ni kwamba licha ya mageuzi yake, jambo moja ambalo halitabadilika ni kwamba watu daima watabaki katika biashara hii. Nimefurahishwa na jinsi itakavyokua katika miaka 20 ijayo kwa teknolojia mpya na njia mpya za mawasiliano.
Je, unaonaje miaka 20 ijayo itakavyokuwa?
JTB: Nadhani ningesema bado tunaichukua hatua moja baada ya nyingine, ingawa, hatua zinaweza kuwa kubwa sasa kuliko ilivyokuwa tulipoanza. Pia nadhani tumejipanga zaidi kukabiliana na miaka 20 ijayo.
Lengo letu kuu litakuwa kujenga, kukuza, na kuimarisha safu ya pili – wanamtandao na wafanyakazi wenye shauku ambao wanaweza kuchukua nafasi kutoka kwetu. Hatuwezi kuwa hapa milele, kwa hivyo tunataka kutoa mafunzo na kujenga kizazi cha pili cha viongozi wenye shauku ambao watabeba urithi wetu mbele.
DSVE: Miaka 20 ijayo itahusiana zaidi na viongozi 20 wa kizazi kijacho kuliko sisi wawili. Ni matumaini yangu makubwa kwamba kadiri majukumu yetu yanavyopungua katika kampuni na kadri uwepo wetu unavyopungua jukwaani, ujumbe wetu utakua katika nguvu na shauku. Acha iendelee kuwaka angani bila kukoma; Jiinueni. Wanadamu wanawangoja.